Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 31, 2014

MOURINHO: JEURI YA LUKAKU NDIYO ILIYONIFANYA NIMUUZE.





                                Jose Mourinho.
Baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Chelsea Romelu Lukaku   kujiunga na Everton kocha Jose Mourinho amesema mchezaji huyo hakuwa tayari kupigania namba kwenye kikosi hicho cha jijini London.
Mourinho ameeleza sababu ya kuruhusu mchezaji huyo yaia wa Ubelgiji kuondoka Stanford Bridge kuwa Lukaku alitaka kuchezea Chelsea na awe chaguo la kwanza jambo ambalo ni gumu kwenye kikosi chake.
Kocha huyo raia wa Ureno  amezidi kutetea uamuzi wa kumuuza nyota huyo kwakusema baada ya Everton kupeleka dau zuri wamelazimika kummuuza mchezaji huyo ili klabu inufaike kwa kupata fedha za kuwasaidia.
Lukaku ambaye amejiunga na Everton maarufu kama Toffiz kwa uhamisho ulioweka rekodi kwa wachezaji wenye umri wa miaka 21 alifunga magoli 15 msimu uliopita wa ligi katika klabu hiyo akitokea Chelsea kwa mkopo.
                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment