Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 27, 2014

ATLETICO MADRID YAREFUSHA MKATABA WAKE NA NIKE HADI 2026.




                                                   Kikosi cha Atletico Madrid  2013/2014.

Mabingwa wa ligi kuu ya Hispania timu ya Atlertico Madrid imerefusha makataba wake na kampuni ya kimarekani ya Nike inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya michezo hadi mwaka 2026.

Taarifa zilizothibitishwa  zimemkariri rais wa timu hiyo Miguel Angel Gil Marin akisema wanashukuru kuendelea na mkataba  mrefu zaidi na kampuni hiyo na hilo ni jambo mhimu sana kwao.

Kwa mara ya kwanza kampuni ya Nike kuingia makubaliano  ya kutengeneza vifaa vya michezo na klabu hiyo ilikuwa mwaka 2001 na mkataba huu mpya utaifanya Nike ifikishe miaka 25 na rais wa Atletico Madrid amesema  hayo ni mafanikio kwao.

Katika msimu uliopita wa La liga timu ya Atletico Madrid chini ya kocha Diego Simeoni ilitwaa ubingwa wa ligi hiyo ya Hispania  kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996.

                         Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment