Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 16, 2014

BAADA YA MSOTO MREFU CHELSEA DEMBA BA AJIUNGA NA BESIKTAS YA UTURUKI.




                    Ba akishangilia goli kwa imani ya dini yake ya Kiisilaam.

Mshambuliaji wa Chelsea raia wa Senegal Demba BA amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Besiktas klabu hiyo ya Uturuki na mchezaji mwenyewe wamethibitisha.

Ba mwenye umri wa miaka 29 katika kipindi cha miezi 18 amefunga magoli 14 kwenye michezo 51 aliyoichezea Chelsea maarufu mama The Blues tangu ajiunge nayo mwezi wa kwanza mwaka jana akitokea Newcastle United.

Besiktas inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki imethibitisha usajili huo kupitia tovuti yake huku Demba Ba akithibitisha kuhamia kwenye kikosi hicho kupitia ukurasaa wake wa Twita.

                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment