Luiz Felipe Scolari.
Uongozi wa shirikisho la soka nchini
Brazil CBF umethibitisha kwamba aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo Luiz
Felipe Scolari amejiuzulu nafasi yake.
Taarifa hiyo imesema Scolari na
wasaidizi wake wote wameachia ngazi kwakujiuzulu kufuatia matokeo mabovu kwenye
michezo yao miwili ya mwisho waliyocheza katika fainali za mwaka huu za kombe
la dunia zilizomalizika juzi.
Makamo wa raisi wa shirikisho hilo
la soka nchini Brazil Marco Polo del Nero amesema wanamshukuru Scolari na
wasaidizi wake kwa mchango walioutoa kwenye timu ya taifa licha ya kutopata
matokeo waliyoyatarajia.
Scolari aliyewahi kuifundisha timu
ya taifa ya Ureno pamoja na klabu ya Chelsea ya nchini England jana
aliwasilisha barua katika ofisi za shirikisho la soka nchini Brazil ya
kujiuzulu nafasi hiyo licha ya mkataba wake ulikuwa unamalizika mara baada ya
kuisha kwa fainali za kombe la dunia.
Katika fainali za mwaka huu ambapo
ubingwa umeenda kwa Ujerumani baada ya kuifunga Argentina katika hatua ya
fainali goli 1 kwa 0 Brazil ya Scolari iliambilia nafasi ya nne kufuatia kipigo
cha magoli 3 kwa 0 ilichokipata kutoka kwa Uholani.
Kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa
tatu Brazil hiyo hiyo ikiweka rekodi kwa
kufungwa magoli mengi zaidi katika mchezo mmoja ambapo ilinyukwa magoli 7 kwa 1
na Ujerumani katina nusu fainali.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment