Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 12, 2014

WAKALA YA YAYA TOURE AWASHUTUMU WANAOMNYIMA NYOTA HUYO TUZO.






Wakala wa Yaya Toure amedai kuwa sababu ya kiungo huyo wa Manchester City kutoshinda tuzo zozote kubwa ni kutokana na  rangi  ya ngozi yake.

Wakala huyo, Dmitri Seluk amesema kiungo huyo raia wa Ivory Coast angeweza kumaliza katika nafasi ya juu zaidi ya nafasi ya tatu katika tuzo za PFA na FWA za mchezaji bora wa mwaka, na pia zaidi ya nafasi ya 12 katika tuzo ya Ballon d'Or, kama angekuwa mzungu.
Luis Suarez alishinda tuzo ya PFA na FWA akifutiwa na Eden Hazard na Steven Gerrard katika kura zilizopigwa.

Seluk ameongeza kusema: "Amesikitishwa kidogo na hali ilivyo. Messi ni mchezaji mzuri katika historia ya soka na ninawaheshimu sana Ronaldo na Ribery. Yaya anawaheshimu wachezaji hao. Lakini ni vigumu kwa Mwafrika katika tuzo hizi. FIFA inahitaji kubadilisha kitu hapa."

Seluk pia amekataa kuhakikisha kuwa Yaya atakuwepo City msimu ujao, akisema: "Kama klabu kubwa kama PSG au Real Madrid wakipanda dau kubwa, Man City watalazimika kuamua kitakachofuata
."

                                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment