Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 30, 2014

YAYA:NITAENDELEA KUWEPO MAN CITY KADRI ITAKAVYOWEZEKANA.



Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City Yaya Toure amebainisha kuwa anataka kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu kadri ya itakavyowezekana.

 
Yaya Toure. 


Yaya mwenye umri wa miaka 31 amesema anafuraha kubakia kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya England na hasa baada ya kujiunga na timu hiyo inayojiandaa na msimu mpya wa 2014-2015.

kiungo huyo ambaye hapo awali alikuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na PSG ya Ufaransa amewataka mashabiki wa Manchester City kutoamini maneno yasiyotoka kwenye kinywa chake lakini yatakayozungumzwa na wakala wake ni ya kweli.

Toure ambaye ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Enfglannd msimu uliopita amesema anajisikia furaha kuungana na wenzaje kwenye maandalizi ya msimu mpya chini ya kocha Manuel Pellegrini.

                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment