Pages

Ads 468x60px

Friday, July 18, 2014

NAHODHA WA MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI,PHILIPP LAHM ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA.



                     Lahm aliyeshikilia kombe la dunia.

Kiungo wa mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bayern Munich Philpp Lahm ametangaza kustaafu kichezea timu ya taifa lake la Ujerumani ambao ni mbabingwa mara nne wa kombe la dunia.

Uamuzi wa Lahm mwenye umri wa miaka 30 kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa umewashtua wengi ikiwa ni siku chache baada ya Ujerumani kutwaa ubingwa wa dunia kwakuifunga Argentina goli 1 kwa 0 katika hatua ya fainali nchini Brazil.

Kiungo huyo ambaye ameiongoza vyema Ujerumani kutwaa taji kubwa la kwanza tangu mwaka 1996 ambapo nchi hiyo ilinyakua ubingwa wa mataifa ya Ulaya amesema amemtaarifu kocha wa  timu ya taifa Joachim Low juu ya uamuzi wake huo.

Nahodha huyo ambaye hucheza nafasi ya ulinzi wa pembeni kwenye timu yake ya taifa  amecheza michezo 113 na kuwa mchezaji wa 4 aliyecheza michezo mingi zaidi kwenye kikosi hicho nyuma ya Lothar Matthaus michezo 150, Miroslav Klose michezo 137 na Lukas Podolski michezo 116.

Lahm ni miongoni mwa nyota waliotwaa ubingwa wa Ulaya wakiwa na timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 2004, 2008 ,2012, 2006, 2010  na pia kombe la dunia mwaka huu wa 2014.

                              Mkule.blogsport.com 

No comments:

Post a Comment