Pages

Ads 468x60px

Friday, July 11, 2014

HUYU NDIYE MRITHI WA ZIZU KATIKA BENCHI LA UFUNDI LA REAL MADRID.




Uongozi wa mabingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu timu ya Real Madrid imemteua Fernando Hierro kuwa kocha msaidizi kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane ambaye alikuwa kwenye benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Carlo Ancelotti.

Tovuti ya mabingwa hao wa bingwa Ulaya kwa vilabu  imethibitisha kuwa Hierro mwenye umri wa miaka 46 ataungana na jopo la ufundi la kikosi cha kwanza cha Real Madrid timu ambayo amewahi kuichezea michezo 416 na kushinda vikombe vinne vya La liga.

Zidane mwenye umri wa miaka 46 alidumu na Real Madrid msimu uliopita  akiwa msaidizi wa Carlo Ancelotti nakufanikiwa kutwaa kombe la 10 la klabu bingwa ulaya  tangu washinde taji hilo mwaka 2002 ambaye Real iliifunga Bayern Leverkusen magoli 2 kwa 1.

Zidane maarufu kama Zizu mwezi uliopita aliteuliwa kuwa kocha wa Real Madrid Castilla ambayo inashiriki ligi ya Seguna Division B.

Hierro enzi hizo akiwa na uzi wa Real madri.


Zizu akiwa na bosi wake,Carlo Ancelotti.



Zizu akiwa na uzi wa Real madrid enzi zake...

 
mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment