Pages

Ads 468x60px

Monday, July 28, 2014

HUYU NDIYE KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA SERBIA.

                                                          Dick Advocaat.
 
Shirikisho la soka nchini Serbia limemtangaza  mdachi Dick Advocaat kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sinisa Mihalovic kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Advocaat mwenye umri wa miaka 66 amechukua nafasi hiyo baada ya kocha Sinisa kufukuzwa kuifundisha timu hiyo mwaka 2013 kufuatia matokeo mabaya.

Kocha huyo mpya amewahi kuiongoza timu ya taifa ya Uholanzi mwaka 1994 na korea Kusini kwenye michuano ya kombe la dunia ameeleza kuwa ameshuhudia michezo 10 ya kikosi hicho hivyo anajua ni nini cha kufanya ili kuboresha kikosi hicho.

Advocaat pia amewahi kuvinoa vikosi vya PSV na Zenit St Petersburg aliisaidia timu ya Uholanz, Scotland pamoja na Urusi kushinda mataji mbalimbali ya nyumbani ambayo yamepelekea kuaminiwa na mataifa mengi katika soka


                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment