Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 26, 2014

DEJAN LOVREN MBIONI KUFANYIWA VIPIMO TAYARI KWAKUJIUNGA NA LIVERPOOL.





                                     Dejan Lovren.

Baada ya klabu ya Liverpool kufikia makubaliano ya kumsajili mlinzi wa Southampton Dejan Lovren,mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya mwishoni mwa wiki hii.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kufanyiwa vipimo hivyo kabla ya Liverpool kurejea Anfield wakitokea kwenye ziara yao nchini Marekani ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu England.
Lovren ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Chile ameeleza kuwa anafurahia kwenda kuichezea timu hiyo huku akiamini ni muda muafaka wa kukamilisha ndoto zake za muda mrefu katika soka.
Liverpool mpaka hivi sasa wamewasajili wachezaji wanne akiwemo Rickie Lambert na Adam Lallana kutoka Southampton, mchezaji Emre Can wa Bayer Livakuzen pamoja na Lazar Markovic wa Benfica.

                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment