Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 15, 2014

ANAUZWAAAAAAAAAAAAAAAA.




                                                 Demba Ba

Klabu ya soka ya Chelsea inajiandaa kumuuza mshambuliaji Demba Ba kwenda timu ya Besiktas ya Uturuki kwa kiasi cha Euro milioni 13 uongozi wa timu hiyo umethibitisha.

Raia huyo wa Senegal tangu ajiunge na Chelsea akitokea Newcastle United mwezi wa kwanza mwaka jana amefunga magoli 14 katika michezo 51 aliyocheza na ujio wa Diego Costa ndani ya Chelsea unatajwa ni sababu ya mchezaji huyo kuuzwa.

mwenyekiti wa Besiktas Fikret Orman amesema usajili huo ukikamilika waviarifu vyombo vya habari lakini dau lililotajwa la paundi milioni 13 huenda likapungua.

Ba ambaye licha ya kutopangwa mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Chelsea msimu uliopita alikuwa akifanya vyema kila alipopata nafasi na uwepo wa wachezaji Fernando Toress na Samwel Eto’o umekuwa sababu ya yeye kuwa chaguo la tatu kwa kocha Jose Mourinho.

                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment