Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 23, 2014

HUYU NDIYE MRITHI WA PUYOL BARCA.




                                                         Jeremy Mathieu.

Timu ya Fc Barcelona imethibitisha kufikia makubaliano ya kumsajili mchezaji Jeremy Mathieu raia wa Ufaransa kutoka Valencia kwa dau la Euro milioni 20  na kupewa mkataba wa miaka minne.

Barcelona imekuwa katika mawindo ya usajili kwa muda mrefu ikimtafuta mlinzi wa kati kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Carles Puyol aliyestaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita na Mathieu mwenye umri wa miaka 30 amekuwa mbadala wake.

Fc Barcelona imethibitisha kupitia tovuti yake  kwamba imefikia makubaliano na Valencia  kumsajili raia huyo wa Ufaransa  anajiandaa kusaini mkataba wake wa miaka 4 na manunuzi yake ni Euro milioni 20 lakini thamani yake itakuwa Euro milioni 50.

Mathiew alianzia soka lake katika timu ya Sochaux lakini pia amewahi kuvaa jezi ya Touluse kabla ya kujiunga na Valencia msimu wa 2009  akicheza michezo 177 na kufunga magoli 7 kwenye kikosi hicho.

                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment