Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 22, 2014

RASMI KINDA JEMES RODRIGUEZ ATUA REAL MADRID NA KUPEWA JEZI NO,10.





Tayari jezi ya nyota mpya wa Real Madrid  Jemes Rodriguezi ipo sokoni.

Klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid leo imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa mshabuliaji Jemes Rodriguez kutoka Monaco ya Ufaransa kwa kiasi cha Euro milioni 88 kwa mkataba wa miaka sita  na kupewa jezi namba 10.

Madrid ambayo hivi karibuni imekamilisha uhamisho wa kiungo Ton Kroos kutoka Beryn Munich ya Ujerumani imetangaza kupitia tovuti yake kuwa imekamilisha usajili wa raia huyo wa Colombia baada ya kufaulu vipimo vya Afya.

Rodriguez ambaye alijiunga na Monaco mwaka jana akitokea Fc Porto ya Ureno kwa ada ya Euro milioni 45 mkataba wake utamalizika mwaka 2020 msimu uliopita alifunga magoli 9 katika michezo 34 aliyocheza akiwa na Monaco.

Rodriguez mwenye umri wa miaka 22 alianzia soka lake katika klabu ya Envigado na katika fainali za kombe la dunia  mwaka huu aliisadia Colombia kuingia robo fainali kabla ya kuondoshwa na Brazil na huku yeye akiibuka mfungaji bora kwa kufunga magoli 6.

    Hapa Rodriguez akiwa na Cristiano Ronaldo.

Hapa Jemes Rodriguez akisalimiana na kocha Carlo Ancelotti.
                           

                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment