kikosi cha Mbaspo academy cha mkoani Mbeya.
Timu ya soka ya Mbaspo academy ya
mkoani Mbeya imekwama kushiriki mashindano ya Rolling stone yanayotaraji kuanza
tarehe 15 ya mwezi huu jijini Daresalaam.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya kulea
na kukuza vipaji vya soka nyanda za juu kusini mwa Tanzania Haroub Suleiman
amesema jitihada zao za kushiriki zimeshindikana licha ya juhudi kadhaa
walizozifanya.
Haroub ambaye ni katibu mkuu wa
chama cha kandanda mkoani Mbeya amesema hadi kufikia jana walikuwa na kiasi cha
shilingi milioni 4 pekee kati ya milioni 8.5 ambazo zinahitajika kwaajili ya
gharama ya safari na chakula na malazi.
Mkurugenzi huyo ambaye amekuwa
mstari wa mbele kuhamasisha soka la vijana kupitia taasisi hiyo yenye makazi
yake makuu mjini Mbeya amesema kama watapata mdhamini wa kuwasaidia kiasi
kilichopungua wapo tayari kuondoka kwenda jijini Daresalaam kushiriki michuano
hiyo.
Amebainisha kuwa kikosi cha Mbaspo
kwasasa kinaendelea kujifua kwaajili ya mashindano mbalimbali ambayo wamekuwa
wanaalikwa na wachezaji wanamorali kubwa ya kucheza soka.
Mkurugenzi wa Mbaspo academy Haroub Suleiman.(aliyesimama katikakati)
Wakati huo huo timu ya Ruaha academy ya mkoani Iringa ambayo tayari ipo jijini Daresalaam kwaajili ya kushiriki mashindano ya Rolling stone imeendelea kujifua na leo imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tabata Future nakufanikiwa kushinda magoli 4 kwa 0.
Michuano ya Rolling stone ambayo
hufanyika kila mwaka kwakushirikisha mataifa mbalimbali ya ukanda wa Afrika
mashariki na kati inaanza kutimua vumbi tarehe 15 ya mwezi huu wa 7 jijini
Daresalaam.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment