Rais wa Tff Jamali Malinzi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameandaa futari kesho (Julai 17 mwaka huu) kwa
wadau mbalimbali wa mpira wa miguu.
Shughuli hiyo itafanyika
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo waalikwa wataanza kuwasili
saa 11.30 jioni.
Waalikwa katika futari hiyo
wametoka katika makundi mbalimbali.
Makundi hayo ni wadhamini, klabu za Ligi
Kuu na Daraja la Kwanza za Dar es Salaam ambazo zitawakilishwa na watu wawili
wawili.
Viongozi wa zamani wa TFF,
Said El Maamry, Leodegar Tenga, Muhidin Ndolanga, Athuman Nyamlani, Mwina
Kaduguda, Michael Wambura, Fredrick Mwakalebela na Ashery Gasabile.
Wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa TFF waliopo Dar es Salaam, Wizara ya Michezo na Ofisa Elimu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.
Vyama shiriki; TWFA, TAFCA,
TASMA, SPUTANZA, FRAT ambavyo vitawakilishwa na watu watatu watatu, viongozi wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Baraza la Michezo la
Taifa (BMT), wahariri wa habari za michezo, Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA) na Polisi kanda Maalumu- Dar es Salaam.
Wajumbe wa kamati ndogondogo
za TFF waliopo Dar es Salaam, wazee wa Simba na Yanga- watano kutoka kila
klabu, timu ya Serengeti Boys, klabu ya Saigon, Bodi ya Ligi Kuu, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Wakuu wa wilaya za Dar es Salaam, wabunge wa Dar es Salaam,
Meya wa Dar es Salaam, Meya wa Kinondoni, Meya wa Ilala na Meya wa Temeke.
Waalikwa wengine ni Omari
Abdulkadir, Amin Bakhresa, Harudiki Kabunju, Hamis Kissiwa, Ismail Aden Rage,
Masoud Sanani, Jamal Bayser, Hassan Dalali, Imani Madega na Mbaraka Igangula.
BONIFACE WAMBURA
OFISA
HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment