Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 30, 2014

VAN GAAL AIONYA MANCHESTER UNITED.





                              Van Gaal akiwa na vijana wake.

Wakati Manchester United ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kocha Louis van Gaal ameionya timu hiyo kutotarajia mafanikio ya haraka kwakuwa itawachukua muda wa miezi mitatu kuzoea ufundishaji wake.

Kocha huyo wazamani wa timu ya taifa ya Uholanzi  akizungumza akiwa nchini Marekani amesema katika kila klabu aliyowahi kuifundisha  amekuwa na kawaida ya kutumia miezi mitatu kwa wachezaji kuzoea mfumo anaofundisha nahuwa si jambo rahisi.

Van Gaal amesema huwa anapenda kufundisha akili kuelewa na sio miguu jambo mhimu kwa wachezaji kufahamu ni kufanya kile anachowaelekeza nakuongeza kwamba nahilo si jambo rahisi.

Van Gaal ambaye alichukua nafasi ya kocha David Moyes amekuwa na matokeo mazuri katika michezo yake ya kwanza ya kirafiki akiwa na Manchester United na leo timu hiyo imeifunga Inter Milan kwa mikwaju ya penati 5 kwa 3.

                                   Wilfred Zaha kazini.

      Nyota mpya wa Manchester United Ander Herrera akimkabili nyota wa Inter Milan leo.


                    Nyota mpya wa Manchester United Ander Herrera mzigoni.
                                                             Mata kazini.
                                                              Vijana wa Van Gaal mzigoni.

                                         Vijana wa Man United wakisikiliza maelezo.
                                         Hapa vijana wa Van Gaal wakipongezana.
                 
                             Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment