Pages

Ads 468x60px

Monday, July 28, 2014

THE CREANS YAPATA PIGO,OKWI AUMIA.

                                                            Emmanueli Okwi.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda  Emmanuel Okwi ameondolewa katika kambi ya kikosi hicho kinachojiandaa kucheza mchezo marejeano dhidi ya Mauritania kuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani.
Okwi ambaye anaichezea  Yanga ya jijini Dare-salaam ataukosa mchezo huo unaotaraji kuchezwa tarehe 3 ya mwezi ujao  kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyonga  timu ya Uganda Creans Milutin Sredojevic ‘Micho’ amethibitisha.
Mshambuliaji huyo alitolewa kipindi cha pili katika mchezo wa awali ambapo Uganga ilishinda magoli 2 kwa 0 pambano lililochezwa katika uwanja wa Nelson Mandela uliyopo Namboole nchini Uganda.
Wachezaji wa Uganda Creans wanaocheza soka nchini Kenya Godfrey Walusimbi na Geoffrey Kizito wa Gor mahia na nyota wa Tusker fc Khalid Aucho wamejiunga na wenzao kambini jana usiku  tayari kwa safari ya Alhamisi ya wiki hii kuelekea Mauritania.

Nyota wa Uganda Creans waliopo kambini hadi sasa  ni : Benjamin Ochan, Robert Odongkara, Denis Iguma, Nicholas Wadada, Denis Okot, Savio Kabugo, Richard Kassaga, Andrew Mwesigwa, Isaac Isinde, Kyambadde, Farouq Miya and Brian Majwega, Godfrey Walusimbi, Geoffrey Kizito, Robert Ssentongo, Brian Umony and Hamis Kizza.

                            Mkule.blosport.com
 

No comments:

Post a Comment