Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 17, 2014

BREKING NEWZZZZZZZZZZZZ...TONI KROOS HUYOOOOOOOOO SANTIAGO BERNABEU AMWAGA WINO WA MIAKA 6.





                                      Toni Kroos.

Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich imetangaza rasmi kuwa mchezaji Toni Kroos amekamisha usajili wa kujiunga na mabingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu timu ya Real madrid.

Kroos ambaye alikuwa anawaniwa na vilabu mbalimbali vya barani Ulaya amesaini mkataba wa miaka 6 ya kuichezea Real Madrid inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama La Liga.

Mkataba huyo utamfanya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 kusalia Santiago Bernabeu hadi mwaka 2020.

Mkurugenzi wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema wanamshukuru Toni kwa mchango wake wote tangu ajiunge nao akiwa na miaka 16 na kucheza zaidi ya michezo 170 kwenye kikosi cha kwanza kuanzia september 2007.

Kroos ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Ujeruamni kilichotwaa ubingwa wa dunia nchini Brazil mwaka huu leo  anataraji kutambulishwa  rasmi kuwa mchezaji wa Real Madrid kwa mashabiki na vyombo vya habari.

                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment