Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 12, 2014

BONDIA FRANCIS CHEKA ASOMEWA SHITAKA LA SHAMBULIZI LA AIBU KWA MENEJA WAKE WA BAR MKOANI MOROGORO.






BINGWA  wa ngumi za  super middle Weight   bondia Francis Cheka maarufu kwa jina la SMG  amesomewa shitaka linalomkabili katika mahakama ya  hakimu mfawidhi mkoa wa morogoro juu ya kufanya shambulizi la aibu kwa meneja wake  wa baa  ndg.Bahati Kabanga mjini Morogoro.

Akisoma shitaka hilo Mwendesha mashitaka Bi Aminatha Mazengo amesema kuwa Cheka anakabiliwa na shitaka la shambulio la aibu ambapo anashitakiwa kwa mujibu wa kifungu namba miambili arobaini na moja( 241)kifungu cha kumi na sita (16) cha mwaka elfumbili na mbili (2002) cha makosa ya jinai

Na kuwa mnamo tarehe mbili mwezi wa saba mwaka elfumbili na kumi na nne maeneo ya ukumbi wa vijana social Mjini Morogoro bila ya halali alimshambulia  Bw Bahati.

Cheka amekana shitaka hilo na  hivyo   Hakimu anayesimamia kesi hiyo Bw Said Diwani Msuya amesema kuwa dhamana kwa mshitakiwa iko wazi kwa wadhamni wawili ambapo kila mmoja ametakiwa kuwa na dhamana ya shilingi  Millioni moja .

Kesiu hiyo imehirishwa hadi tarehe ishirini na tatu mwezi wa saba mwaka elfumbili na kumi na nne.

H
                                      Hapa Cheka akiwa Ulingoni(mwenye bukta nyekundu.)

mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment