Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 22, 2014

ARSENAL YANASA SAINI YA MLINDAMLANGO NAMBA 1 WA TIMU YA TAIFA YA COLOMBIA.




                                              David Ospina

Wakati  vita vya usajili vikiendelea kushika kasi katika vilabu mbalimbali barani Ulaya,timu ya Arsenal imefanikiwa kuinasa saini ya mlinda mlango wa kimataifa wa Colombia David Ospina kwa uhamisho wa euro milioni 4.4.

Ospina mwenye umri wa miaka 25 anayeichezea timu ya OGC Nice amesaini mkataba wa miaka 4 na kwa hivi sasa bado yuko mapumzikoni baada ya kushiriki michuano ya kombe la duni iliyomalizika mapema mwezi huu nchini Brazil.

Mlinda mlango huyo ambaye alitoa mchango mkubwa katika timu ya taifa ya Colombia, baada ya kufuzu vipimo vya afya atakuwa akilipwa mshahara wa  paundi elfu  60,000 kwa wiki.

Ospina amekuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Asernal msimu huu baada ya kuwasajili kwa  Alexis Sanchez na Mathieu Debuchy  huku akitarajiwa kuleta changamoto kwa mlinda mlango nambari moja  wa kikosi hicho Wojciech Szczesny.


                                          David Ospina.

              Mlindmlango namba 1 wa Arsenal Wojciech Szczesny.
                                              
                                                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment