Dunga.
Shirikisho la soka nchini Brazil CBF
limiethibitisha kuwa Dunga ndiye kocha mpya wa timu yao ya taifa kuchukua
mikoba ya Luiz Felipe Scolari aliyeachia ngazi hivi karibuni kufuatia kikosi
ncha nchi hiyo kushindwa kutwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka huu.
Ndunga ambaye alifanikiwa kushinda
kombe la dunia mwaka 1994 akiwa nahodha wa Brazil kuteuliwa kwake itakuwa mara
ya pili kuifundisha timu ya taifa hilo maarufu kama Selecao baada ya kuwahi
kuinoa timu hiyo kati ya mwaka 2006 -2010.
Dunga mwenye umri wa miaka 50 mara
baada ya kuthibitishwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil amesema bado
Brazil inauwezo wa kushindana na kutwaa
mataji na anaamini wataonyesha ubora wao.
Mlinzi huyo wa zamani wa Brazil
amesema hawapaswi kufikiria kwamba walikuwa bora bali wao ni bora hadi
sasa kwasababu wanavijana wengi wenye
vipaji vikubwa na yapo mataifa
yanayotamani kuwa na timu kama ya Brazil.
Dunga amesema mchezo wa mpira wa
miguu sio mchezo wa mtu mmoja au watu wawili maarufu bali unahitaji ushirikiano wa wachezaji wote
katika timu.
Katika maisha yake ya soka Dunga
amewahi kuichezea timu ya taifa ya Brazil michezo 60 akishinda michezo 42 na
kikosi hicho huku kikosi chao kikifungwa
michezo 6 pekee.
Licha ya kushinda kombe la Copa
America mwaka 2007 na kombe la mabara mwaka 2009 akiwa kocha mkuu wa timu ya
taifa ya Brazil Dunga alikosolewa sana kabla ya kutimuliwa mwaka 2010 baada ya kufungwa na Uholanzi hatua ya robo
fainali.
Baada ya uteuzi wa kocha huyo mpya kikosi cha kwanza
cha timu ya taifa ya Brazil kinaraji kutangazwa mwishoni mwa mwezi wa 8 mwaka
huu kabla ya kuikabili Colombia,na Ecuador nchini Marekani.
Dunga akiwa na kikosi cha Brazil kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika ya Kusini.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment