Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 16, 2014

SAMATA NA ULIMWENGU WAWASILI KUIKABILI MSUMBIJI.





                             Samata na Ulimwengu.

Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji hao wamefikia hoteli ya Courtyard, Seaview Upanga na leo jioni walitarajiwa kufanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij wakati wakiwasubiri wachezaji wenzao ambao wapo kambini mkoani Mbeya.

 Naye kiungo Mwinyi Kazimoto anayecheza soka katika klabu ya Almarhiya ya Qatar atawasili nchini kesho saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.

Wakati huo huo kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, taifa Stars kitawasili jijini Dar es Salaam kesho saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kikitokea jijini Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.

                         Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment