Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 15, 2014

WALCOTT MBIONI KUREJEA DIMBANI.




                   Walcott akitolewa uwanjani kwa machela.


Wakati msimu mpya wa ligi kuu ya England ukitaraji kuanza mwezi ujao mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Arsenal Theo Walcott  yupo mbioni kurejea uwanjani baada ya kukosa michezo ya  mzunguko wa pili wa ligi hiyo msimu uliopita.

Walcott ambaye aliumia msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Tottenham ambapo Arsenal ilishinda magoli 2 kwa 0 amesema kwasasa anaendelea kupona vizuri na anamatumaini ya kuanza msimu mpya akiwa amepona.

Nyota huyo raia wa Uingereza ambaye alishindwa kulitumikia taifa lake katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil amebainisha kuwa jeraha la goti lililokuwa linamsumbua linaendelea vizuri na ameshaanza mazoezi ya viungo.

Walcott mwenye umri wa miaka 25 kurudi kwakwe uwanjani kutasaidia kuimarisha zaidi safu ya ushambuliaji ya Arsenal baada ya hivi karibuni kumsajili Alex Sanchez kutoka Fc Barcelona ya nchini Hispania.



Walcott akimiliki mpya kwenye mmoja ya michezo ya ligi msimu uliopita.
                                
                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment