Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 15, 2015

KIKOSI CHA SOUTHAMPTON CHAPATA PIGO,WANYAMA AUMIA.



                                   Victor Wanyama akiwa amelala baada ya kuumia.

Klabu ya soka ya Southampton ya Uingereza itamkosa kwa majuma 6 nyota wake raia wa Kenya victor wanyama baada ya kuumia kwenye mchezo wa kufuzu mzunguko wa 4 wa  michuano ya  FA.

Kocha mkuu wa klabu ya hiyo Ronald Koeman amethibitisha kuwa wanyama ameumia nyama za paja hivyo kwenye mchezo  dhidi ya Ipswich town hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda huo .

Kutokana na maumivu hayo wanyama mwenye umri wa miaka 25 atakosa michezo ya timu yake dhidi ya Liverpool,Newcastle united ,Swansea city ,QPR pamoja na west ham United.

Nyota huyo ambaye amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi ya koeman akifanikiwa kuanza kwenye michezo 24 ,anaungana na nyota wengine Morgan Schneiderlin na Toby Alderweireld ambao pio majeruhi.

                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment