Pages

Ads 468x60px

Friday, January 16, 2015

PIGO KUBWA ARSENAL,ARTETA & DEBUCHY KUKAA NJE MIEZI 3.



          Mikel Arteta aliyekaa chini,hapa ilikuwa katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund.

                Mathieu Debuchy akiwa katika mmoja ya mikikimikiki na kikosi cha Arsenal.

 Klabu ya soka ya Arsenal imepata pigo kubwa baada ya wachezaji wake Mikel Arteta na Mathieu Debuchy kulazimika kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Arteta mwenye Miaka 32, amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu baada ya kuumia muda mrefu wakati Debuchy amefanyiwa upasuaji kwenye Bega aliloumia  juma lililopita.

Mara baada ya kujiunga na Arsenal mwanzoni mwa Msimu akitokea newcastle, Debuchy aliumia na kuwa nje kwa  Miezi Mitatu na hali hiyo imemfanya aichezee Arsenal michezo 14 tu .

Arteta, ambae mara ya mwisho kuichezea Arsenal ni Novemba 26 ilipoifunga Borussia Dortmund magoli 2-0, amefunga magoli 16 katika Michezo 136 aliyoichezea Arsenal tangu ajiunge nayo akitokea Everton Agosti 2011.

                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment