Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 14, 2015

RAIS WA GUINEA KUWALIPIA TIKETI ELFU AROBAINI MASHABIKI WA NCHI HIYO KWENYE MICHUANO YA AFCON 2015.



                             Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema.

Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema , amesema kuwa yeye mwenyewe atalipia jumla ya tiketi elfu arobaini kwa ajili ya wapenzi wa soka nchini mwake ili waweze kuhudhuria mechezo ya Kombe la Mataifa Afrika.

Michuano hiyo inayotarajiwa kuaza  jumamosi,nchini humo  ilitangazwa kufanyika nchini humo baada ya kuthibitishwa kuwa hayatafanyika nchini morocco iliyojitoa kutokana na tishio la ugonjwa wa ebola.

 Rais Obiang amesema anaona ni wajibu wake na wengine wenye uwezo kununua tiketi jambo ambalo litatoa wito kwa mashabiki na kujaza viwanja watakatoa hamasa kwa timu shiriki.

Fainali za mataifa ya afrika mwaka huu zitaanza kutimua vumbi januari 17 na kumalizika februali 8 huku wenyeji wa michuano hiyo wakifungua dimba kwa kucheza na timu ya taifa ya congo.


                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment