Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 14, 2015

LIPULI FC VITANI LEO MKOANI RUVUMA KUSAKA ALAMA TATU ZA KUIPIKU AFRIKAN SPORTS (FDL).



                         Kikosi cha Lipuli fc cha mkoani Iringa kitakachoikabili Mlale jkt ya Ruvuma.

Klabu ya soka ya lipuli ya mkoani iringa inataraji kushuka katika dimba la majimaji mjini songea jioni ya leo kucheza dhidi ya maafande wa jkt mlale katika muendelezo wa michezo ya ligi daraja la kwanza.
Katibu msaidizi wa wanapaluhengo hao lonjino Malambo  amesema kuwa baada ya kuvuna alama 2 kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya African lyon na majimaji wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa leo .
Katika mchezo uliopita lipuli ikiwa ugenini ilitoka sare ya goli 1 kwa 1 na majimaji na kujiongezea alama 1 huku ikihitaji kushinda leo na kujiwekea mazingira mazuri ya kupanda kucheza ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015-16.
Mpaka sasa majimaji inaongoza kundi A ikiwa na alama 32 ikifuatiwa na African sports ya Tanga yenye alama 29,lipuli ina alama 28,friends rangers alama 26,tessema alama21 na kimondo ambayo leo itacheza na African lyon ikimaliza nafasi ya 5 na alama zake  20.
Wakati huohuo kikosi hicho cha Wanapaluhengo kitaendelea kupata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki wao ambao wamekuwa wakiongozana na kikosi nhicho kila mahala kwenye michezo yake ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
Kikundi cha mashabiki wa Amsha popo ni kati ya vikundi vilivyojizoea umaarufu kwa ushangiliaji wao tangu kuanza kwa msimu huu wa FDL.

                                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment