Pages

Ads 468x60px

Monday, September 1, 2014

LAURENT KOSCIELNY ATEMWA KATIKA KIKOSI CHA UFARANSA.





Mlinzi wa klabu ya Arsenal Laurent Koscielny ameenguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachocheza michezo ya kirafiki mwezi huu dhidi ya Hispania na Serbia baada ya kuumia jana kwenye mchezo dhidi ya Leciester City.
Shirikisho la soka la nchini Ufaransa limethibitisha kuwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 ameenguliwa kikosini kutokana na kuumia kichwa kwenye pambano la jana la ligi kuu ambapo Arsenal ilitoka sare ya goli 1 kwa1 na wapinzani wao.
Baada ya kuachwa kwa Koscielny  nafasi yake imechukuliwa na nyota mpya wa Fc Barcelona Jeremy Mathieu ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Valencia akiwa amecheza michezo miwili katika timu ya taifa.
Katika mchezo wa jana mara baada ya kuumia kwa Koscielny ambaye aligongana na mchezaji wa Leicester City Jeffrey Schlupp nafasi yake ilichukuliwa na Calum Chambers dakika ya 26.

                                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment