Pages

Ads 468x60px

Monday, September 1, 2014

JERAHA LA GOTI LAMWEKA NJE GIUSEPPE ROSSI.




                                         Giuseppe Rossi.
Klabu ya Fiorentina imethibitisha kuwa mshambuliaji Giuseppe Rossi anataraji kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kushoto lilokuwa linamsumbua.
Nyota huyo raia wa Italia ambaye alianza kusumbuliwa na jeraha hilo tangu Oktoba mwaka 2011 wakati anaichezea Villareal ya Hispania hali hiyo inatishia kipaji chake hasa baada ya kutibiwa takribani mara nne.
Rossi mwenye umri wa miaka 27 aliposajiliwa na Fiorentina mwezi januari mwaka 2013 amekuwa akiandamwa na majeraha  ya goti kwa mara kadhaa kiasi cha kukaa nje ya uwanja kwa miezi minne kabla ya kurejea mwezi wa kwanza mwaka huu.
Rossi amefunga magoli 17 katika michezo 25 aliyocheza kwenye klabu hiyo na akikosa michezo 52 kutokana na majeraha tangu asajiliwe kutoka Villareal.

                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment