Pages

Ads 468x60px

Tuesday, September 9, 2014

TISHIO LA RIBERY KUADHIBIWA ENDAPO ATAGOMA KUICHEZEA UFARANSA BAADA YA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA BAYERN YALONGA



                                        Frank Ribery.

Uongozi wa klabu ya Bayern Munich umesema hawawezi kumlazimisha mshambuliaji wao Frank Ribery kubadili uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa  baada ya rais wa Uefa Michel Platini kumtaka mchezaji huyo kubadili uamuzi wake.
Mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema suala la Ribery kubadili msimamo wake wa kustaafu soka la kimataifa ni la kwake mwenyewe  na wao kama klabu wamemruhusu kufanya maamuzi anayoona ni sahihi kwake.
Kiongozi huyo ametolea mfano wa aliyekuwa nahodha wa mabingwa wa dunia kwasasa Ujeruman Philipp Lahm kuwa alipoamua kustaafu soka la kimataifa aliongea na kocha Joachim Low hivyo na Ribery anapaswa kuongea na kocha wa timu yake ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps.
Hivi karibuni rais wa shirikisho la soka barani Ulaya ambaye ni raia wa Ufaransa Michel Platini alikaririwa akisema atamwadhibu Frank Ribery kutocheza michezo 3 katika klabu yake ya Bayern Munich kama ataitwa kwenye timu ya taifa na kukataa.

                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment