Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 11, 2014

PIGO KWA LIVERPOOL STURRIDGE KUKAA NJE WIKI 6.



                     Daniel Sturridge akigangwagangwa na daktari wa timu yake ya taifa ya England.

Klabu ya Liverpool ya Uingereza inataraji kumkosa mshambuliaji wake Daniel Sturridge kwa muda wa majuma sita baada ya kuuumia mwenyewe akiwa mazoezini kwenye timu yake ya taifa.
Kocha mkuu wa Liverpool Brendan Rodgers amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo  alieumia mazoezini akiwa kwenye timu yake ya taifa ya Uingereza alibainika kuumia  saa 36 baada ya kucheza dakika 89 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Norway juma lililopita.
Sturridge anataraji kukosa michezo 6 ya ligi ukiwemo dhidi ya watani wao wa jadi Everton utakaochezwa tarehe 27 ya mwezi huu,pambano dhidi ya Middlesbrough  wa kombe la ligi pamoja na mchezo wa kwanza hatua ya makundi klabu bingwa Ulaya.
Kuumia kwa  Sturridge aliyejiunga na Liverpool akitokea Chelsea  kunatoa nafasi kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Mario Ballotelli  kuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kucheza mchezo wake wa kwanza kesho wakati  Liverpool itakapoikaribisha Aston Villa.

                                         Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment