Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 11, 2014

RIBERY AKAIDI AGIZO LA PLATINI KUMTAKA ARUDI KUITUMIKIA TIMU YA TAIFA.



                                           Frank Ribery.

Mshambuliaji wa Bayern munich Frank Ribery amesema kamwe hawezi kubadili uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa baada ya kutangaza uamuzi huo siku kadhaa zilizopita.
Ribery mwenye umri wa miaka 31 uamuzi wake wa kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa umekosolewa na rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini ambaye hivi karibuni amesema anaweza kumwadhibu winga huyo ikiwa atagoma kuchezea timu ya taifa kama ataitwa na kocha Didier Dischamps.
 Pamoja na kushambuliwa vikali na rais huyo ambaye ni raia wa Ufaransa Ribery ambaye alikosa fainali za kombe la dunia mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na jeraha la nyama za paja amesema kwasasa akili yake ameielekeza kwenye klabu yake ambayo inakibarua cha kutetea taji la Bundesiliga msimu huu.
 "I want to focus completely on Bayern Munich in the future. That's all I want to say about the matter. I am not going to get involved in all the politics surrounding my decision."

Mchezaji huyo amesema ameshazungumza na kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps juu ya uamuzi wake wa kustaafu na wamekubaliana  hivyo hana mpango wa kurudi kuichezea timu ya taifa.
Katika michezo 81 aliyoichezea timu ya taifa ya Ufaransa mchezaji huyo amefunga magoli 16

                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment