Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 10, 2014

Anelka kujiunga na FC Pune City.



                                   Nicolas Anelka.

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid,PSG,Chelsea na Arsenal Nicolas Anelka anajiandaa kujiunga na klabu ya FC Pune City baada ya kuamua kughairi kujiunga na Mumbai City.
Licha ya mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa kuvivutia vilabu mbalimbali vya nchini India lakini yeye ameamua kujiunga na timu ya Mumbai City  ya  Maharashtra nchi iliyopo magharibi mwa India.
Anelka mwenye umri wa miaka 35 tangu afukuzwe  na timu yake ya zamani yaWest Bromwich Albion  ya England  amekosa klabu ya kuchezea licha ya mara kadhaa kuhusishwa na mipango ya kujiunga na timu mbalimbali ikiwemo za nchini Brazil.
Mkongwe huyo ambaye pia amewahi kuvichezea vilabu vya Juventus na Manchester City  mwaklishi wake amekuwa kwenye mazungumzo na timu ya FC Pune City  kwaajili ya kukubaliana  juu ya usajili huo.

                                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment