Pages

Ads 468x60px

Monday, September 8, 2014

ENGLAND YAENDELEA KUANDAMWA NA MAJERUHI,HENDERSON HATARINI KUIVAA USWIS LEO.



                                  Jordan Henderson

Kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza Jordan Henderson  yupo kwenye hatihati ya kuukosa mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Ulaya  mwaka 2016 dhidi ya Uswis unataraji kuchezwa leo .
Habari kutoka katika kambi ya timu ya taifa ya Uingereza zimeeleza kuwa kiungo huyo yupo kwenye hatari kutocheza pambano hilo litakalochezwa kwenye uwanja wa St.Jacob Park  mjini Basel baada ya kuumia kifundo cha mguu akiwa mazoezini.
Nyota wa Manchester City Jemes Milner  huenda  akachukua nafasi ya Henderson licha ya  mchezaji Fabian Delph anayeichezea Aston Villa kuonyesha uwezo mkubwa kwenye pambano la hivi karibuni ambapo Uingereza ilicheza na Norway.
Mbali na Jordan Henderson  kuwa kwenye hatarai ya kuukosa mchezo huo wa leo kocha wa Ungereza Roy Hodgson  amewaengua mlindamlango Ben Foster na kiungo Jack Colback  kutokana na kuwa majerihi.
                           
                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment