Pages

Ads 468x60px

Tuesday, September 2, 2014

ANDY MURRY ATINGA ROBO FAINALI YA US OPEN.



                                                 Andy Murry.

Bingwa wa zamani wa mashindano ya wazi ya Marekani anayeshikiria nafasi ya 9 duniani kwa upande wa wanaume  Andy Murray amefuzu  kuingia hatua ya robo fainali  ya mashindano hayo baada ya kumshinda mpinzani wake Jo-Wilfried  Songa.
Murray,  ambaye katika mashindano hayo anashikiria nafasi ya nane amepata ushindi huo kufuatia kumshinda Songa kwa seti  7kwa5, seti7kwa5,  seti 6kwa4  ikiwa ni miaka mitatu ipite tangu afuzu kuingia hatua ya robo fainali mwaka 2010.
Mchezaji nambari moja duniani Novak Djokovic amefuzu kuingia hatua ya robo fainali kufuatia kupata ushindi kutoka kwa mpinzani wake Philipp Kohlschreiber ambaye ni mwenyeji wa mashindano hayo.
Kwa upande wa wanawake mwanadada Serena Williams anajiandaa kukabiliana na  Flavia Pennetta kwenye hatua ya robo fainali ya mashindano ya wazi ya Marekani baada ya kumfunga mpinzani wake Kaia Kanepi kwa seti 6kwa3,seti 6kwa3 kwa dakika65. 

                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment