Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 11, 2014

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA URENO AACHIA NGAZI.



                                                                         Paulo Bento.
 
Shirikirisho la soka nchini Ureno limethibitisha kuwa  aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo Paulo Bento ameachia ngazi baada ya kikosi chake kufungwa na Albania kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016.
Bento mwenye umri wa miaka 45 amefikia makubaliano na shirikisho la soka la nchi hiyo  ya kukatisha mkataba kufuatia kipigo cha goli 1 kwa 0 kutoka kwa  Albania  mapema juma hili na mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi yake umeanza.
shirikisho hilo la soka la Ureno FPF  limemshukuru kocha huyo kwa mchango wake wa kuifundisha timu yao  nakusema wanamatumaini kuwa watapata kocha mwengine atakekuwa na jukumu la kuifundisha timu hiyo siku chache kutoka sasa.
Bento ambaye  alicheza michezo 35 kwenye timu ya taifa ya Ureno  akiwa mchezaji alianza kuinoa Ureno  mwaka 2010 akichukua nafasi ya  Carlos Queiroz ambaye aliachia ngazi kutokana  na kuanza vibaya kwenye michezo ya kufuzu kwa fainali za Ulaya 2012.

                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment