Pages

Ads 468x60px

Monday, September 8, 2014

MAICON KUUKOSA MCHEZO WA KESHO KATI YA BRAZIL NA EQUADOR.



     Mlinzi wa timu ya taifa ya Brazil Doglas Maicon jezi namba 2.


Mlinzi  wa klabu ya AS Roma ya Italia Doglas Maicon ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kinachojiandaa kuikabili Equador  kesho jumanne na nafasi yake kuchukuliwa na nyota wa AS Monaco  Fábio Tavares  maarufu kama Fabinho.
Maicon ambaye alianzishwa na kocha Dunga katika mchezo wa kirafiki  dhidi ya  Colombia ijumaa iliyopita  imeelezwa  anamatatizo ambayo hata hivyo hayajawekwa wazi na kocha wa kikosi hicho kijulikanao kama Selecao.
Taarifa za kuenguliwa kwa mlinzi huyo wa  zamani wa vilabu vya Inter Milan na Manchester City  zimethibitisha mapema  usiku wa kuamkia leo na kocha wa sasa wa Brazil aliyechukua nafasi ya Luis Felipe Scolar.
Mrithi wa Maicon  Fabinho amewasili  asubuhi ya   leo katika kambi ya timu ya taifa ya Brazil  tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Equador.

                 Mrithi wa Maicon katika timu ya Fabinho.
                                
                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment