Pages

Ads 468x60px

Monday, September 15, 2014

ANELKA ATUA RASMI KATIKA LIGI KUU YA NCHINI INDIA.



                                    Nicolas Anelka

Nyota wa zamani wa vilabu vya soka vya  Chelsea , Real Madrid, na Arsenal Nicolas Anelka ametangaza kujiunga na  klabu ya  Mumbai City inayoshiriki ligi kuu ya nchini India baada ya kukaa bila timu tangu aachwe na West Bromwich ya Uingereza.
Anelka mwenye umri wa maiak 35 ametangaza kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twita akisema anamatumaini  kuwa atapewa ushirikiano mkubwa na wachezaji kwenye timu yake mpya  na atahakikisha anacheza kwa kujituma katika michezo atakayocheza.
Mkongwe huyo ambaye amecheza michezo 69 katika timu yake ya taifa ya Ufaransa alianzia soka lake katika  klabu ya PSG kabla ya kujiunga na Arsenal na baadae kuvichezea vilabu vya Real Madrid,Manchester City, Fenerbahce, Bolton, Chelsea, Shanghai Shenhua, Juventus na hatimae  West Bromwich.
Anelka anaungana na wachezaji wengine wakongwe  wanaolipwa pesa nyingi kwa siku  kwenye ligi kuu ya India akiungana na Robert Pires ,Freddie Ljungberg , Alessandro del Piero na David Trezeguet.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment