BENKI ya NMB imeingia mkataba wa
udhamini wa miaka miwili na klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Azam FC ambao
utahusu gharama za usafiri na baadhi za uendeshaji wa timu.
Akizungumza leo makao makuu ya
klabu, Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Mwenyekiti
wa Azam FC Sheikh Said Muhammad Said amesema kwamba mkataba huo unaanza mara
moja.
Sheikh Said amesema kwamba
wanaishukuru NMB kwa kuwapa Mkataba huo na anaamini utaongeza ufanisi katika
klabu yao.
“Tumeupokea kwa furaha Mkataba huu
na tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa NMB kwa kuungana nasi,”amesema.
Akifafanua kuhusu Mkataba huo,
Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Iddrisa Mohammed ‘Father’ amesema NMB itanufaika
kwa kutangazwa kwenye jezi za Azam, mabasi na pia kuweka mabango yao kwenye
Uwanja wa Azam Complex.
“Nembo za NMB zitapamba jezi za Azam
FC kuanzia mazoezini na kwenye mashindano yote, vyombo vyetu vya usaifiri
kadhalika vitawekwa nembo za NMB kama itakavyokuwa kwenye Uwanja wetu a Azam
Complex,”amesema Father.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji
wa NMB, Mark Wiessing amesema mafanikio ya Azam FC ndiyo yaliyowavutia kuingia
nao ndoa hiyo. “Mafanikio ya Azam FC katika soka ya Tanzania ndiyo yametuvuta
kuingia nao ushirika huu,”amesema.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment