Pages

Ads 468x60px

Monday, September 1, 2014

ATLETICO MADRID MBIONI KUKAMILISHA USAJILI Cerci KUTOKA TURINO.



                                           Alessio Cerci.

Mabingwa wa ligi kuu Hispania  maarufu kama La Liga Atletico Madrid  wamekubali kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Alessio Cerci kutoka klabu ya Torino inayoshiriki ligi kuu ya kwao.
Cerci mwenye umri wa miaka 27  anataraji kusaini mkataba wa miaka mitatu  na mabingwa hao baada ya kufuzu vipimo vya afya kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi leo huku akitegemewa kuchukua nafasi ya Diego costa.
Mchezaji huyo ambaye msimu huu alishiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil amekuwa akiwaniwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo klabu ya Arsenal pamoja na Manchester United.
Mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid Jose caminero ameeleza kuwa wamefurahi kufikia makubaliano na mchezaji huyo atakayekuwa msaada mkubwa katika kikosi chao kwenye msimu huu wa ligi kuu Hispania.

                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment