Pages

Ads 468x60px

Monday, September 1, 2014

FALCAO ATUA MANCHESTER UNITED KWA MKOPO.



                                  Radmel Falcao.

Wakati dirisha la usajili barani Ulaya likitaraji kufungwa rasmi usiku wa leo klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na Monaco ya Ufaransa juu ya kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu mshambuliaji Radmel Falcao.
 Falcao ambaye ni raia wa Colombia uhamisaho wake wa kutua Manchester United umegharimu kiasi cha paundi milioni 6  na ataraji kufanyiwa vipimo kabla ya dirisha la usajili kufungwa majira ya saa sita na dakika moja usiku wa leo.
Tangu ajiunge na Monaco ya Ufaransa  kwa paundi milioni 50 mwezi mei 2013 Falcao kwa msimu uliopita amefunga magoli 11 katika michezo 20 aliyocheza na mitatu ya msimu huu .
Falcao ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujinga na Arsenal vyombo vya habari baranu Ulaya vimearifu kuwa kocha wa Manchester United Louis Van Gaal ameanza kumfuatilia mshambuliaji huyo tangu saa 48 zilizopita.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment