Mwanamasumbwi raia wa Marekani Floyd
Mayweather ameendelea kushikilia ubingwa wa WBA na WBC baada ya kumshinda kwa
pointi bondia Marcos Maidana mjini Las
Vegas Marekani.
Mayweather mwenye umri wa miaka 37
ameendeleza rekodi katika miaka 18 ya
maisha yake ya ngumi akicheza michezo 47 bila kupoteza ukilinganisha na
mabondia wengine tangu aanze kushiriki ngumi za kuliwa mwaka 1996.
Bondia huyo ameweka rekodi ya
kushinda michezo 47 kwenye ngumi za kulipwa,akishinda mipambano 26 kwa K.O huku mipambano mitano mikubwa ya dunia
akishikilia ubingwa na kutopigwa pambano lolote.
Akizungumza mara baada ya mchezo
Mayweather mwenye uzito wa kilo 68
amesema hakuamini pale ambapo mpinzani wake alimng’ata kidole chake katika
mzunguko wa nane jambo lilomfanya asitumie sana mkono wake wa kushoto.
Floyd Mayweather factfile
|
Born: 24 February 1977, Grand Rapids, Michigan
|
Amateur record: 84 wins, six defeats. Three-weight Golden Gloves
champion. Bronze medal at 1996 Olympics
|
Turned professional: 11 October 1996
|
Professional record: 47 wins (26 KOs), no defeats. Five-weight world champion
|
Worth: Highest-paid athlete in world in 2012, earning $85m (all
from boxing), and 2014, earning $105m (all from boxing)
|
Ushindi huo umeripotiwa kumpatia
Mayweather takribani dola za marekani
milioni 32 sawa na paundi milioni 19.6 kwa pambano hilo liliokuwa likisubiriwa
kwa hamu kubwa na mashabiki wa masumbwi duniani kote.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment