Pages

Ads 468x60px

Tuesday, September 2, 2014

SCHWEINSTEIGER NAHODHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI.



Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amemteua mchezaji Bastian Schweinsteiger kuwa nahodha mpya baada ya kustaafu kwa nahodha wa awali Philipp Lahm  mwezi uliopita.
Wakati Schweinsteiger akipewa unahodha kocha Joachim Low amesema uamuzi wa kumteua kiungo huyo kuwa nahodha mpya unatokana na sifa ya uongozi akiwa ndani na hata nje ya uwanja hivyo anaimani naye huku msaidizi wake akiwa Manuel Neur.
Kocha huyo amesema benchi la ufundi zima limekuwa na imani na mchezaji huyo mwenye umri wa maiak 30 na akiwa amecheza michezo 100 kwenye timu ya taifa tangu mwaka 2004.
Schweinsteiger  atakosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Argentina  unaotaraji kuchezwa hivi karibuni kutokana na kuwa majeruhi  hivyo mlinda mlango Manuel Neur ambaye ni nahodha msaiodizi atakuwa na  jukumu hilo la kuwaongoza wenzake .
                                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment