Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 17, 2014

KIBARUA CHA OLE GUNNAR HATARINI KUOTA NYASI.



                                 Ole Gunnar Solskjaer.

Kocha wa timu ya Cardiff City Ole Gunnar Solskjaer amekutana na uongozi wa klabu hiyo kwalengo la kufanya mazungumzo juu ya matokeo mabaya waliyoyapata katika  michezo ya Championship.
Kikao hicho kinafuatia  vipigo viwili mfululizo  ambavyo timu hiyo imevipata ndani ya siku nne ikifungwa 1 kwa 0 na Middlesbrough jana jumanne pamoja na ule wa  capitulation  dhidi ya  Norwich ambapo timu hiyo ilifungwa magoli 4 kwa 2.
 Solskjaer mwenye umri wa miaka 41 alichukua mikoba ya  Malky Mackay  January 2 kwaka huu lakini alishindwa kuinusuru timu hiyo  na janga la kushuka daraja katika ligi kuu ya Uingereza.
Mshambuliaji huyo mkongwe  wa Manchester United amesema  anakubali lawama zote zinazoelekezwa kwake  kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata  lakini akisistiza kuwa kikosi hicho kitapata matokeo mazuri hivi karibuni.
Katika michezo 30 aliyoiongoza Cardiff City  kuanzia achukue nafasi hiyo kocha huyo ameshinda michezo 9 akienda sare 5 na kupoteza michezo 16 hali ambayo inatishia kibarua  chake kuota nyasi.

                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment