Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 5, 2014

SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI ALGERIA LATHIBITISHA KOCHA MPYA KUSAINI MKATABA.




                                                                   Christian Gourcuff.


Shirikisho la soka nchini Algeria limetangazwa kuwa kocha mpya wa timu yao ya taifa mfaransa Christian Gourcuff amesaini rasmi mkataba  kuchukua nafasi ya Vahid Halilhodzic aliyejiuzulu baada ya kutolewa kwenye hatoa ya robo fainali ya kombe la dunia.
Uongozi wa shirikisho hilo umesema kocha huyo amekubali kuiongoza Algeria katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015,2017 na pia ataendelea hadi katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi.
Gourcuff mwenye umri wa miaka 59 ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya Lorient atakuwa akishirikiana na nahodha wa zamani wa Algeria Yazid Mansouri ambaye amewahi kumfundisha akiwa Lorient.
Gourcuff aliachia ngazi katika klabu ya Lorient mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuipandisha kutoka ligi ya ngazi ya mkoa na kuipeleka katika ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama League one.
                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment