Kombe la kwanza chini ya Van Gaal.
Kocha mpya wa Manchester
United Louis Van Gaal ameanza kurudisha furaha kwa mashabiki wa timu hiyo baada
ya usiku wa kuamkia leo kuifunga Liverpool magoli 3 kwa1 na kutwaa ubingwa wa
kombe la kimataifa kwa upande wa vilabu.
Taji hilo ambalo ni la
kwanza kwa Van Gaal akiwa kocha wa Manchester United limempa matumaini ya timu
yake kuanza kuimarika ikiwa kwenye michezo ya majaribio nchini Marekani kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Liverpool ndiyo iliyokuwa
yakwanza kupata goli kupitia kwa kiungo Steven Gerald kwa mkwaju wa penalty kabla
ya Manchester United kusawazisha kupitia nahodha wake Wayne Roon huku magoli mengine yakifungwa na Juan Mata
na Jesse Lingard.
Pamoja na kusema ushindi
huo ni furaha ya mashabiki wa United waliyopo marekani na duniani kwa ujumla
Van Gaal amesema baada ya kuwapa nafasi wachezaji wote kucheza juma hili
anataraji kutangaza majina ya nyota ambao hatokuwa nao msimu ujao wa ligi kuu
ya England.
Vikosi vya timu zote vilivyocheza ni hivi hapa.
Manchester United: De Gea, Evans (Blackett 45), Smalling, Jones, Valencia (Shaw 8), Herrera (Lingard 78), Fletcher (Cleverley 45), Young, Mata (Kagawa 69), Rooney, Hernandez (Nani 69).
Liverpool: Mignolet, Kelly, Johnson, Skrtel, Sakho (Toure 74), Gerrard (Lucas 62), Allen (Can 62), Henderson, Coutinho (Peterson 77), Lambert (Ibe 62), Sterling.
Smalling akikabiliana na Skrtel.
United wakishangilia goli kwa pamoja kwenye mchezo dhidi ya Liverpool ambapo Man United ilishinda magoli 3 kwa 1..
Giggs na Van Gaal.
No comments:
Post a Comment