Pages

Ads 468x60px

Monday, August 4, 2014

VIDAL AJUMUISHWA KATIKA KIKOSI CHA JUVE KITAKACHOELEKEA BARANI ASIA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA.




                                        Arturo vidal.

Licha ya kuhusishwa na mipango ya kuhamia Manchester United timu ya Juventus  imemjumuisha kiungo Arturo Vidal  kwenye orodha ya wachezaji 28 katika ziara ya barani Asia kwaajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.
Raia huyo wa Chile amekuwa akihusishwa  kwakiasi kikubwa  kuhamia Manchester United lakini kocha mpya wa Juve  Massimiliano Allegri amekuwa akipuuza habari hizo nakusema Vidal yupo kwenye mipango yake.

Katika  orodha hiyo ya wachezaji watakaotembelea mataifa Indonesia,Australia na Singapore  wamo pia viungo Andre Pirl na Paulo Pogba pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina  Carlos Teves.

Katika Ziara hiyo miamba hao wa Bianconeri watazikabili timu mbalimbali ikiwemo mjumuiko wa wachezaji wa ligi kuu ya Australia jumapili ijayo kabla ya kucheza na Singapore All Stars mjini Singapore Augost 16 mwaka huu.

Kikosi kitakachosafiri hiki hapa...


Walinda mlango: Buffon, Storari, Rubinho, Audero
Walinzi: Bonucci, Motta, Caceres, Chiellini, Ogbonna, Marrone, Blanco
Viungo: Lichtsteiner, Romulo, Pirlo, Marchisio, Vidal, Padoin, Pogba, Pereyra, Evra, Asamoah, Pepe, Vitale
Washambuliaji: Llorente, Tevez, Giovinco, Coman, Buenacasa


Mkule.blogsport.com.

No comments:

Post a Comment