Pages

Ads 468x60px

Monday, August 4, 2014

BARCELONA YATHIBITISHA XAVI KUUMIA MAZOEZINI.





                                            Xavi.

Timu ya Fc Barcelona ya Hispania imethibitisha kuwa kiungo wake Xavi ameumia misuli ya miguu  leo jumatatu akiwa mazoezini kujiandaa na msimu mpya wa 2014/2015.

Tovuti ya klabu hiyo imearifu kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 alilazimika kutoka uwanjani na daktari timu hiyo ndiye atakaetoa taarifa kwamba nyota huyo atarejea lini uwanjani .

Licha ya mara kadhaa kuwepo kwa taarifa kwamba nyota huyo  anayeichezea timu ya taifa ya Hispania anaweza kuihama Barcelona msimu huu wa usajili mkurugenzi wa ufundi wa kikosi hicho Andoni Zubizarreta  mwezi uliopita alithibitisha kwamba wataendelea kuwa nae.

Kiungo huyo alicheza michezo 29 msimu uliopita wa La Liga  nakufunga magoli matatu kisha kuisaidia Barcelona kumaliza katika nafasi ya pili  kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania nyuma ya mabingwa timu Atletico Madrid.

                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment