Pages

Ads 468x60px

Monday, August 4, 2014

MWANAMKE WA KWANZA KUFUNDISHA KLABU YA SOKA BARANI ULAYA KIBARUANI LEO.



                                         Corinne Diacre.

Kocha wa timu ya Cermont Foot inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa mwanamama Corinne Diacre anataraji kuiongoza klabu hiyo kwenye mchezo wake wa kwanza leo jumatatu dhidi ya Brest akiwa kocha  mkuu.

Diacre mwenye umri wa miaka 40 ni mwanamke wa kwanza kufundisha soka la kimataifa kwa klabu na huu utakuwa mchezo kwanza kwake tangu ateuliwe mwezi wa sita kwa mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya mwanamama wa Kireno Helena Costa.
Diacre alichukua nafasi ya Helena ambaye alijiuzulu siku mmoja kabla ya kuanza kibarua cha kuinoa  timu ya Cermont Foot kwakile alichodai  wachezaji waliokuwepo hakuwasajili yeye hivyo rais wa timu hiyo Claude Michy kumpa nafasi hiyo Diacre.

Kwaupande wake Diacre ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa amesema lengo lake kwenye pambano la leo dhidi ya Brest ni kuhakikisha anawaongoza wachezaji katika jukumu lao.

                               Kikosi cha Cermont Foot.

                    Wachezaji wa timu ya Cermont Foot.

                              Mkule.blogsport.com.

No comments:

Post a Comment