Pages

Ads 468x60px

Monday, August 4, 2014

HAYA NDIYO MAKUNDI YA TIMU ZA TAIFA ZITAKAZOCHUANA KWENDA MORROCO 2015.






 Makundi ya timu za taifa zitakazochuana kuwania nafasi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco yamekamilika baada ya kumalizika kwa hatua za awali hapo jana.

Hatua hiyo mhimu imefikiwa baada ya  michezo ya marejeano kumalizika huku mataifa saba yakikata tiketi ya kuingia kwenye makundi ambapo tarehe tano ya mwezi ujao michezo ya mzunguko wa kwanza inataraji kuanza.

Hatua hiyo itaenda hadi tarehe 19 ya mwezi wa 11 ambapo vinara wa kila kundi pamoja na timu tatu bora zitajulikana tayari kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika zinazotaraji kuanaza januari 17 hadi februari 8 mwakani nchini Morocco.

Mataifa saba yamwisho yaliyokata tiketi jana na kuingia hatua ya makundi ni Botswana, Lesotho, Malawi, Mozambique, Rwanda, Sierra Leone na  Uganda.

Yafuatayo ni Makundi ya timu za mataifa mbalimbali yaliyofuzu kuchuana kusaka tiketi ya kwenda Morocco mwakani.

Group A: Nigeria, South Africa, Sudan, Rwanda
Group B: Mali, Algeria, Ethiopia, Malawi
Group C: Burkina Faso, Angola, Gabon, Lesotho
Group D: Ivory Coast, Cameroon, DR Congo, Sierra Leone
Group E: Ghana, Togo, Guinea, Uganda
Group F: Zambia, Cape Verde, Niger, Mozambique
Group G: Tunisia, Egypt, Senegal, Botswana
                              Mkule.blogsport.com                    

No comments:

Post a Comment